Kucheza Michezo kwa Kuwajibika

SportPesa Kenya ni Tovuti ya Kubashiri Michezo ya Mtandaoni na imejitolea kuhamasisha kutabiri kwa kuwajibika.

Ni marufuku kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 18 kucheza michezo ya kutabiri. Kila mtu anapojiunga na kutengeneza akaunti mpya kwenye https://ke.sportpesa.com lazima achague na kuweka tiki kwenye kisanduku kinachoonyesha kuwa yeye ana umri wa miaka 18 na zaidi.

Wito huu wa kutabiri kwa kuwajibika hailengi kuwanyima wachezaji starehe wanayoipata kupitia kutabiri bali ni busara ya kuhakikisha kuwa mchezaji atakuwa na uwezo wa kudhibiti uchezaji wake vizuri.

 

Kudhibiti uchezaji kamari

Kumbuka;

a. Weka bashiri na pesa ambazo unaweza kumudu kupoteza;
b. Zingatia muda unaotumia na pesa unazotumia kubashiri;
c. Kubashiri michezo inafaa kustarehesha na si kuonekana kama njia ya kupata pesa au kuepuka kupata hasara.

Hii ni programu ya kamari ya pesa halisi. Tafadhali cheza kamari kwa kuwajibika na weka dau tu unachoweza kumudu. Kwa usaidizi na usaidizi wa uraibu wa kucheza kamari, bonyeza hapa ke.sportpesa.com/responsible_gaming au tupigie simu kwa nambari: 07079079079 au tembelea responsiblegambling.or.ke kwa msaada wa kuzuia na kutibu tatizo la kubashiri kwa michezo.

Huduma za malipo yetu zimeegemezwa kwenye huduma za pesa za simu. Kisheria, mtu anayetaka kujisajili kwenye huduma hizo za pesa za simu, lazima awe na umri wa miaka 18 na zaidi na awe na kitambulisho sahihi. Malipo ya kutumia cheki au pesa taslimu, huwa tunahitaji uthibitisho wa umri kupitia kitambulisho.

Endapo utahisi au kujua mtoto yeyote anayecheza michezo kwenye majukwaa yetu au kutumia akaunti ya mtu mwengine, tafadhali tufahamishe mara moja kupitia care@ke.sportpesa.com kwa hatua muhimu kuchukuliwa. Maelezo yako yatakuwa ya siri na juhudi yako itashukuriwa.

 

Kuzingatia Mipaka

 

Ukaguzi wa mara kwa mara wa historia ya mteja

Ili kufuatilia shughuli zako za kuweka bet kwenye SportPesa Kenya, tumekuwekea njia rahisi za kuona historia ya shughuli zako za kila mwezi. Bonyeza “Historia ya Bet” kwenye akaunti yako ya https://ke.sportpesa.com kufuatilia bets ulizoweka, pesa ulizotoa na ulizoweka. Aidha, salio lako la SportPesa huonyeshwa daima kwenye upande wa kulia wa skrini yako, unapoingia kwenye akaunti yako.

 

Chaguo la Kujitoa

Huduma ya kujitoa ya SportPesa inakuruhusu kufunga akaunti yako kwa muda fulani.

Wakati umejitoa, hutoruhusiwa kufungua tena akaunti yako au akaunti nyingine mpya.

Utaratibu wa ufuatiliaji utawekwa kwa shughuli yoyote inayohusiana na akaunti yako au ukurasa wako kwenye majukwaa ya kubashiri ya SportPesa. Akaunti zozote mpya zitakazogunduliwa zitafungwa mara moja.

 

Namna ya Kuomba Kujitoa kwenye SportPesa?

Tuandikie barua pepe kwa care@ke.sportpesa.com ili kuomba kufungiwa akaunti yako kwa muda fulani ambao ungependelea.

Baada ya kutuma ombi lako, wawakilishi wetu watawasiliana na wewe kuthibitisha ombi lako na utapokea barua pepe itakayothibitisha kufungwa kwa muda. Baada ya kipindi kumalizika, mteja atahitaji kuomba kufunguliwa upya kwa akaunti yake.

 

Je, hatua za kufunga akaunti zinahusisha nini?

Inahusisha kuangalia salio lililobaki kwenye akaunti yako au bets zozote zilizobakia , na kufunga akaunti, pamoja na kuweka tahadhari juu ya shughuli yoyote itakayohusiana na akaunti hiyo au ukurasa kwenye majukwaa ya kutabiri ya SportPesa.

 

Salio langu kwenye akaunti ya SportPesa Kenya hufanyiwa nini baada ya akaunti kufungwa kwa muda?

Kama kuna salio lolote, tutawasiliana na wewe ili uzitoe au utupatie kibali ya kuwa unataka pesa zile zibaki katika akaunti yako.

 

Nini kitakachotokea kwa bets nilizoweka ambazo bado hazijahitimishwa?

Bets zozote ambazo hazijashughulikiwa zitapata kushughulikiwa kwenye matokeo ya tukio hilo. Kama bet yako imeshinda, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya Huduma kwa Wateja ili kupanga jinsi malipo ya ushindi wako yatafanyizwa.

 

Nifanye vipi ikiwa bado naweza kuingia kwenye akaunti yangu ya SportPesa baada ya kipindi cha kujitenga kuanza?

Kama bado unaweza kuingia kwenye kurasa na huduma zozote za SportPesa baada ya kupokea ujumbe wa kuanza kwa kipindi cha kujitenga mwenyewe, tafadhali tujulishe mara moja.

Tuandikie kwa care@ke.sportpesa.com ukitujulisha kuhusu uwezo wako wa kuingia kwenye akaunti yako na kupata huduma za SportPesa. Usipotujulisha kuhusu hili, basi hatutakuwa na wajibu wowote wa kisheria kwako au kwa mtu mwengine kama unaweza kuweka bet kupitia majukwaa ya SportPesa, baada ya kujitenga.

Betslip

Namba za Paybill

Nambari yako ya akaunti/kumbukumbu inapaswa kuwa nambari yako iliyosajiliwa.

  • 955100 au 5212121
  • 955100 au SPORTPESA

Huduma kwa Wateja

Tunatoa huduma angalifu kwa wateja masaa 24 kwa wachezaji wa SportPesa.